Wednesday, 12 June 2013

KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY

Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.

Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki

Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.


SHIWATA yandaa Tamasha la Kimataifa Dar.


MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa Tamasha la Kimataifa la Michezo mbalimbali litakalofanyika Juni mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tamasha hilo limeandaliwa ili kupata fedha za kujenga nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.


Mwenyekiti wa SHUWATA, Caasim Taalib alisema jana kuwa kutakuwa na michezo na burudani mbalimbali kutoka Tanzania, India, Marekani, Uingereza, Ujerumani, China watakaonesha ustadi wa kucheza katika utamaduni wa nchi zao.


Taalib alisema pia kutakuwa na michezo mipya iliyobuniwa na mtandao huo kama SHIWATA Basketball, SHIWATA Football ambayo inachezwa na ngongoti pia kutakuwa na ngoma, kwaya,Bongo Fleva, dansi, mieleka na michezo mingine ambayo itatoa burudani ya kutosha.


Alisema pamoja na wanachama 185 wa SHIWATA kuamua kuchangisha sh. 200,000 kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo,mtandao huo umeamua kutafuta fedha zaidi kwa njia ya matamasha na filamu ili kuwapunguzia mzigo wa kujichangisha.


Mwenyekiti Taalib alisema mapato ya tamasha hilo yatawanufaisha wanachama 185 ambao tayari wameonesha nia ya kujenga nyumba hizo kupitia filamu iitwayo Kisufuria iliyokwisha chezwa na sasa inahaririwa.


Alisema matamasha kama hilo yanatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Morogoro,Ruvuma, Tanga na Zanzibar ili kujenga nyumba 1,000 kama inavyokusudiwa.


"Nyumba tano zilizojengwa katika awamu ya kwanza na nyumba 180 zinazotarajiwa kuanza kujengwa awamu ya pili Julai mwaka huu, tunawahimiza wanachama wote kuchangia ujenzi wa nyumba zao ili waweze kufaidika kwa fedha zitakazokusanywa kutokana na filamu ma matamasha yaliyoandaliwa"alisema Mwenyekiti Taalib.
Tuesday, 11 June 2013

SHIWATA YA BADILI JINA RASMI
Mwenyekiti wa iliyokuwa SHIWATA ambayo sasa itajulikana kama Mtandao wa Wasanii Tanzania, Bw.Twalib akipokea cheti cha usajili wa mtandao huo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego. Pichani juu: Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw.Ghonche Materego, akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi cheti kipya cha usajili viongozi wa lililokuwa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) ambalo kwa sasa litajulikana kama Mtandao wa Wasanii Tanzania

Msanii na Mjumbe kutoka iliyokuwa SHIWATA mbayo sasa inakuwa mtandao wa wasanii, Ahmed Olotu a.k.a Mzee Chilo, akitoa shukrani kwa Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw.Materego.

Sehemu ya wanachama wa SHIWATA waliohudhuria hafla hiyo ya kukabidhiiwa ChetMadabida kuwakopesha Sh. Bil. 7 wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)

3a

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida ameahidi kuwakopesha Sh. bil.7  Wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kwa ajili ya kuendeleza fani hiyo.
Akifungua tamasha la wasanii Mastaa chipukizi zaidi ya 400 lililofanyika Jumapili katika ukumbi wa Starlight Hotel,Madabida alisema kwa kuwa SHIWATA inawanachama 7,000 kila mmoja atakopeshwa sh. mil. Moja zitakazomsaidia kuimarisha sanaa yake  iwe ya kisasa zaidi.
Madabida alisema taasisi ya Informal Sector Workers Union ambayo  yeye ni mlezi,huwakopesha wajasiriamali kwa riba nafuu hivyo itasaidia kuwatoa hapo walipo kwani wasanii nchini bado masikini wanahitaji kusaidiwa ili kujikwamua kimaisha.
Amesema Rais Jakaya Kikwete yupo pamoja na wasanii nchini hivyo wajione wapweke na wasikate tamaa badala yake waendelee na jukumu lao na kuelimisha na kuburudisha jamii.
Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) alisema atachangia kulima barabara ya kwenda katika kijiji cha wasanii Mkuranga ambako mpaka sasa nyumba 20 zimejengwa.
Amesema wanaobeza muziki wa kizazi kipya hawaendani na wakati kwa sababu kila enzi ina zama zake hivyo zama hizi ni za muziki wa vijana hayo ni mabadiliko ya dunia nzima.
Madabida ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi vilionesha sanaa zao.
Katika tamasha hilo wasanii wakongwe wa bongo flava , Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na mwigizaji maarufu nchini Bi. Hindu walifanya maonesho katika tamasha hilo likiwa na Kauli Mbiu ya Kilio cha Msanii.
 Tamasha hilo ambalo lilipata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) viongozi kutoka Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania walishiriki katika tamasha hilo.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib amesema tamasha la mwezi Juni mwaka huu litafanyika Mkuranga ambako na viongozi wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa wachukue fomu za kushiriki tamasha hilo