Tuesday 11 June 2013

Madabida kuwakopesha Sh. Bil. 7 wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)





3a

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida ameahidi kuwakopesha Sh. bil.7  Wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kwa ajili ya kuendeleza fani hiyo.
Akifungua tamasha la wasanii Mastaa chipukizi zaidi ya 400 lililofanyika Jumapili katika ukumbi wa Starlight Hotel,Madabida alisema kwa kuwa SHIWATA inawanachama 7,000 kila mmoja atakopeshwa sh. mil. Moja zitakazomsaidia kuimarisha sanaa yake  iwe ya kisasa zaidi.
Madabida alisema taasisi ya Informal Sector Workers Union ambayo  yeye ni mlezi,huwakopesha wajasiriamali kwa riba nafuu hivyo itasaidia kuwatoa hapo walipo kwani wasanii nchini bado masikini wanahitaji kusaidiwa ili kujikwamua kimaisha.
Amesema Rais Jakaya Kikwete yupo pamoja na wasanii nchini hivyo wajione wapweke na wasikate tamaa badala yake waendelee na jukumu lao na kuelimisha na kuburudisha jamii.
Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) alisema atachangia kulima barabara ya kwenda katika kijiji cha wasanii Mkuranga ambako mpaka sasa nyumba 20 zimejengwa.
Amesema wanaobeza muziki wa kizazi kipya hawaendani na wakati kwa sababu kila enzi ina zama zake hivyo zama hizi ni za muziki wa vijana hayo ni mabadiliko ya dunia nzima.
Madabida ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi vilionesha sanaa zao.
Katika tamasha hilo wasanii wakongwe wa bongo flava , Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na mwigizaji maarufu nchini Bi. Hindu walifanya maonesho katika tamasha hilo likiwa na Kauli Mbiu ya Kilio cha Msanii.
 Tamasha hilo ambalo lilipata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) viongozi kutoka Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania walishiriki katika tamasha hilo.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib amesema tamasha la mwezi Juni mwaka huu litafanyika Mkuranga ambako na viongozi wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa wachukue fomu za kushiriki tamasha hilo





No comments:

Post a Comment